THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA WATU WA CHINA

Mkurugenzi Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad amesema upatikanaji wa huduma ya dawa muhimu katika wodi za wazazi umefikia asilimia 96 na wazazi wamekuwa wakipata huduma bila usumbufu.

Amesema Bohari Kuu ya dawa hivi sasa imeimarika na wamekuwa wakisambaza dawa hizo katika Hospitali na vituo vya Afya kwa wakati kwa mujibu ya mahitaji yao.

Mkurugenzi Zahrani ameeleza hayo Ofisini kwake Maruhubi baada ya Wizara ya Afya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba venye thamini ya zaidi ya shilingi milioni 420 kutoka Serikali ya Watu wa China.

Amesema kuimarika kwa huduma ya dawa na vifaa tiba, ni juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wafadhili wengine wa maendeleo katika kuwapunguzia wananchi umasikini.

“Bohari Kuu hivi sasa imejaa dawa na tumeboresha sana huduma katika wodi za wazazi hasa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja,” alisisitiza Ndugu Zahrani.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa alisema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mazingira ya kuzihifadhi dawa hizo katika vituo vya Afya na kuhakikisha zinawafikia walengwa.

Alisema msaada uliotolewa na Serikali ya China, ikiwa ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, sehemu kubwa ni kwa ajili ya wagonjwa wa maradhi ya kuambukiza, sindikizo la damu na sukari ambapo hulazimika kuzitumia kwa muda mrefu na bei zake ni ghali.

Akimkabidhi Waziri wa Afya msaada huo, Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema nchi yake itaendeleza mashirikiano ya kihistoria yaliyoanzishwa na waasisi wa nchi mbili hizi Abeid Amani Karume na Maotse Tung kwa faida ya wananchi wake.

Ameahidi kuendelea kutoa mashirikiano zaidi katika uchumi wa Zanzibar kwa kuimarisha miundo mbinu na kusaidia vifaa tiba na dawa za aina mbali mbali.

Nae Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru China kwa misaada inayotoa kwa Zanzibar na hasa sekta ya afya ambayo imesaidia kuboresha upatikanaji wa huduma katika Hospitali na vituo vya afya.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar