Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi amewataka wamiliki wa hoteli kuajiri wafanyakazi wenye ujuzi katika fani ya ukarimu na utalii baadala ya kuajiri ndugu zao wasio na ujuzi wowote na kuwalipa ujira mdogo hali inayochangia kuzorotesha huduma za utalii mkoani hapo.

Alisema wahudumu walio wengi katika hoteli hizo wamekuwa kero katika utoaji wa huduma kwa watalii pindi wanapotembelea kuja kuona vivutio vya utalii vilivyopo mkoani hapo.

Ametoa raia hiyo jana wakati akifunga mafunzo hayo kwa jumla ya wahitimu 74 yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST unaotekelezwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku tatu kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta ya ukarimu na utalii ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya jumla ya wahitimu 74 waliopewa mafunzo ya siku tatu katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST Mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa katika sekta hiyo ili kukidhi mahitaji ya soko, pamoja na kukuza hadhi ya huduma za malazi zilizopo chini ya kiwango. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskas Mwiru (kulia).

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Constantine Mushi akizungumza na wahitimu kabla ya kufunga jana mafunzo hayo fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya wahitimu 74. Wengine ni Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki (kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii, Paskaz Mwiru (kulia)

Mratibu wa Mradi wa SPANEST nchini, Godwell Meing’ataki akizungumza na   wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.

Baadhi ya wahitimu waliohitimu jana mafunzo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji pamoja na upishi katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika Mkoani Mbeya kwa muda wa siku tatu na kuhudhuriwa na jumla ya washiriki 74.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...