Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali tukio la kubakwa kwa binti wa miaka saba (jina limehifadhiwa) mkazi wa kata ay Kitanzini, mwanafuzi wa darasa la awali shule ya SUN Academy iliyoko kata ya Kwakilosa, manispaa ya Iringa.

Wizara imesikitishwa na taarifa za awali kuwa mtoto alibakwa katika mazingira ya shule mahali ambapo tunategemea pawe salama kwa mtoto kuishi. 

Wakati wote Serikali imekuwa ikisisitiza walezi wa watoto kuhakikisha wanalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ubakaji kwani vitendo hivi vimekuwa vikitaarifiwa kuwahusisha watu wa karibu wanaomzunguka mtoto katika familia, shuleni na jamii.

Wizara inapongeza vyombo vya habari vyote vinavyoibua matukio ya ukatili, kwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utekelezaji wake unahusisha wadau wote nchini.

Wizara inamini kuwa Polisi kwa kutumia weledi na umahiri wao watashirikiana na wananchi, walezi, walimu na marafiki wa mtoto, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafichuliwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Wizara inawakumbusha wazazi na walezi kuwa vitendo vya ukatili ukiwemo ubakaji dhidi ya watoto wa kike havikubaliki katika nchi yetu kwani vitendo hivyo vinatia doa kubwa taifa letu. Natoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kuwafichua waliohusika na ubakaji wa mtoto aliyeripotiwa kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.


Erasto T. Ching’oro
Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...