THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM ZAZIDI KUKAMILIKA.

Makonda atembelea hospitali ya Koica Chanika leo jijini Dar es Salaam.
Hospitali ya Koica Chanika ya Mama na Mtoto inatarajia kuzinduliwa Juni mwaka huu, ambayo inawezo kuendesha oparesheni nne kwa siku.

Hospitali hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini ambapo kujengwa hospitali hiyo kulitokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na Balozi wa Korea Kusini nchini.

Akizungumza wakati alipotembea hospitali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa hospitali hiyo ni mkombozi kwa wanawake na watoto kutokana na kuwa vifaa vya kisasa.

Amesema azma ya serikali ya awamu ya tano ni ya kuhakikisha wananchi wanyonge na masikini wanapata huduma za afya zilizo bora inatimia.

Makonda amesema hakuna kitu kinachoshindikana kama viongozi kufanya kazi za kujitoa kwa wananchi hasa katika sekta ya afya ambayo ndio msingi wa maisha ya watanzania.

Amesema hospitali hiyo ina hadhi yake kutokana na kuwa na vifaa vya kila aina zote ambapo hakuna mama atakayepoteza maisha kutokana na kujifungua ikitokea ni mipango ya Mungu.

Makonda amesema wanawake wakiwa na ujauzito walikuwa wanafikiri huduma wakati wa kujifungua lakini serikali ya awamu ya tano imeweka kipaumbele chini ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk.John Pombe Magufuli.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa kujengwa kwa hospitali hiyo kutapunguza msongamano katika hospitali ya Amana.Amesema kutokana na vifaa huduma ambazo zitatolewa katika Hospitali hiyo kwa mama na mtoto zitakuwa ni za kiwango cha juu.
Mkuu wa Wilaya , Mjema amesema kuwa moja huduma hizo ni kuwa na mashine za kisasa za kufulia ambazo zinaweza kufua kilo 70 kwa saa.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema.

Majengo ya hospitali hiyo kama yaonekanavyo pichani, iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini,ampapo inatarajiwa kuzinduliwa Juni 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelekezo ya vifaa kutoka kwa Daktari wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akitazama baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyofungwa katika hospitali hiyo,alipotembelea mapema leo kuangalia vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Koica Chanika, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vifaa vya kisasa ambavyo tayari vimeishafungwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar.