THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

AIRTEL NA MAENDELEO BENKI WAZINDUA HUDUMA ZA MIKOPO KWA VIKOBA KUPITIA SIMU.

Airtel Money na Maendeleo Benki kuviwezesha Vikundi vya Vikoba nchini
Vikundi vya vikoba kupata njia ya kisasa na salama zaidi ya kuendesha shughuli zao za kifedha

Airtel Tanzania kwa kushirikiana na benkiya Maendeleo leo wamezindua huduma mpya ijulikanayo kamaTimizaVikoba yenye lengo la kuviwezesha vikundi vya vikoba nchini kutumia njia ya kisasa na salama itakayorahisisha ukusanyaji wa michango, kutoa mikopo na marejesho ya mikopo kwa urahisi kabisa.

Huduma hii yaTimiza Vikoba inawawezesha wateja wa Airtel walio katika vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50 kupata huduma za kifedha masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu kwa kupiga *150*60# na kisha kuingia kwenye menu ya Airtel Money na kusajili kikundi na kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki, kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote pale kwa usalama na urahisi zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Bi Beatrice Singano Mallya alisema” huduma ya Airtel Money imekuwa ikiongoza kwa huduma za kibunifu na kisasa zaidi na leo hii tunazindua ushirikiano wa kipekee na benki ya Maendeleo kupitia huduma ya Airtel Money ili kuwawezesha wafanyabishara katika vikundi vya Vikoba nchi nzima kufanya miamala yao ya kifedha kwa njia salama, uhakika na urahisi zaidi.

Huduma hii italeta uwazi na kuwawezesha vikundi vya vikoba kuhakiki taarifa zao kwa kupata taarifa za miamala mbalimbali kwa wakati kupitia simu zao za mikononi. Tunaamini huduma hii itachochea wafanyabiashara bila kujali maeneo walioko kujiunga na kutengeneza vikundi vya vikoba ili kunufaikana kukuza biashara zao
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba akibadilishana makabrasha na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Beatrice Singano baada ya kusaini makubalianao ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Vikoba kwa ajili ya kutoka mikopo kwa vikundi vidogo bila dhamana
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Beatrice Singano na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba wakisaini makubaliano ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Vikoba kwa ajili ya kutoka mikopo kwa vikundi vidogo bila dhamana
Mkurugenzi wa Mawasiliani wa Kampuni ya Airtel, Beatrice Singano akizungumza wakati wa kusaini makubalianao ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Vikoba kwa ajili ya kutoka mikopo kwa vikundi vidogo bila dhamana baina kampuni hiyo na Maendeleo Bank jijini Dar es Salaam jana
Askofu Mkuu wa KKKT, Alex Malasusa akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubalianao ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Vikoba kwa ajili ya kutoka mikopo kwa vikundi vidogo bila dhamana baina kampuni ya Airtel na Maendeleo Bank jijini Dar es Salaam jana.