Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queen kwa lengo la kuiwezesha timu hiyo kuwa na vifaa bora vitakavyowawezesha kuendelea kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi 

Vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na viatu vya mpira pair 20 na socks pair 40 vitawawezesha wachezaji hao kuondoka na changamoto ya vifaa vya michezo hususani viatu bora vya kuchezea mpira ambavyo ni nyenzo muhimi katika mchezo wa soka.

Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kwa niaba ya timu ya Kilimanjaro Queens, Mwenyekiti wa soka la wnawake Amina Karuma alisema “ Tunajisikia furaha kupokea vifaa hivi na nawapongeza sana Airtel kwa kutimiza ahadi yao yakutupatia vifaa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kukuza soka la wanawake nchini.

 Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea kukua kwa soka la wanawake kwa kushirikisha timu  za wasichana katika michuano ya Airtel Rising Stars kila mwaka na kwa kupitia michuano hii tumeweza kupata vipaji tunavyoviona leo katika timu zetu za wanawake.

“Tunawahakikishia vifaa hivi vitatusaidia saana kwani viatu vya mpira ni nyenzo muhimu sana lakini pia ni moja kati ya changamoto kubwa kwa wachezaji wetu. Tunayo mipango mingi na michuano mbalimbali iliyopo mbele yetu na tumejipanga kufanya vizuri lakini pia kujiandaa vyema kwa michuano ya AFCON inayotegemea kuanza Februari Mwakani. “Aliongeza Karuma
Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania, Amina Karuma, jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusadia timu ya taifa ya wanawake ya Kilimanjaro Queens, ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchini. Kulia ni Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkomwa na Nahodha, Sophia Mwasikili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...