Jumanne Aprili 25, 2017 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London.

Ibada hiyo ilifanyika kama sehemu ya kuadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola, Tanzania hufanyiwa maombi maalum kanisani hapo katika siku hii adhimu kila mwaka.

Pamoja na kusoma maandiko matakatifu, Ibada hiyo ilihusisha maombi maalum kwa ajili ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli na Serikali yake, Mahakama na Bunge kama mihimili mikuu ya Amani na Mshikamano wa Taifa la Tanzania na Wananchi wote wa Tanzania ndani na nje ya Nchi.
Ubalozi wa Tanzania London Uingereza unawatakia kheri Watanzania wote waishio Uingereza na Jamhuri ya Ireland katika maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Taifa letu.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt Asha-Rose Migiro, akiwa amewaongoza Watanzania waishio Uingereza kushiriki Ibada Maalum ya kuliombea Taifa iliyofanyika katika Kanisa maarufu la Westminster Abbey jijini London leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...