Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika
kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.
Ameyasema hayo hivi
karibuni wakati alipomtembelea Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista
Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.
Akielezea lengo la ziara hiyo, Balozi Cooke alisema Serikali
yake inataka kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha inajipanga kukabili
na kurejesha hali pindi yanapotokea
maafa.
“Masuala ya maafa
yapo nchi nyingi ikiwemo kwetu Uingereza ingawa mafuriko na ajali za moto
zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu mara kadhaa.”Alisema Balozi.
Aliongeza kuwa, Serikali ya Uingereza imevutiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali
ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na kuwasaidia wananchi na mali zao pindi
yanapotokea maafa.
Kwa upande wake, Waziri Mhagama alimpongeza Balozi huyo
kuona umuhimu wa kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia nchi kwa namna
mbalimbali.
“Nishukuru kipekee kwa ujio wako na kuona umuhimu wa kuunga
mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika maswala mazima ya maafa na
kumhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari na itajiandaa kuwaunga mkono kwa utayari
wa kuisaidia nchi”Alisema waziri Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge,
Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa
Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alipomtembelea waziri Ofisini kwake Bungeni
Dodoma
Balozi wa Uingereza Nchini
Mhe.Sarah Cooke akiongea jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipomtembelea Ofisini
kwake Bungeni Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta
jambo na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alimtembelea Ofisini kwake
Bungeni Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...