Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MVUA kubwa iliyoambata na upepo mkali,imekata mawasiliano ya miundombinu ya barabara eneo la Buyuni, na kusababisha wakazi kutoka kata ya Vigwaza na Mwavi jimbo la Chalinze,kupata shida.
Hali hiyo inasababisha wakazi hao,kuvushwa kwa kupata msaada wa kubebwa mgongoni na shingoni kwa gharama ya sh.3,000 na 2,000 na pikipiki kupitishwa kwa sh.5,000 huku magari yakishindwa kupita kabisa.
Baadhi ya wakazi hao,akiwemo Zaina Zuberi aliekuwa akienda Mwavi,alisema wapo katika hali ngumu.
“Mvua hapa bado haijanyesha,maji haya yanatokea maeneo ya Msoga huko na kufika huku daraja la  Mbiki,Buyuni na kukatiza katika hii barabara,sipati picha mvua ikipiga hapa kwa mwezi huu”
MBUNGE wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akiangalia barabara kutoka Vigwaza-Mwavi iliyoharibika vibaya eneo la Buyuni hali inayosababisha magari kushindwa kupita.

 Mkazi wa Mwavi ,Zainab Zuberi akivushwa  kwenye maji yaliyokata barabara eneo la Buyuni,kwa kubembwa shingoni .
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,akizungumzia kero ya kuharibika kwa baadhi ya  miundombinu ya barabara kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha,ambapo mvua iliyonyesha april 7 na 8 imesababisha kuharibu barabara ya Vigwaza-Buyuni-Mwavi na ya Milo-Kitonga-Ruvu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...