BENKI ya Exim imepata faida ya Tsh bilioni 83.6 (kabla ya kodi) kwa mwaka wa fedha 2016 ikiwa imejumuisha faida ya Tsh bilioni 46.4 ya kuuza hisa ilizowekeza. Faida itokanayo na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kibenki ni Tsh 37.2 Bilioni.

Mapato yatakanayo na riba yaliongezeka kwa asilimia 25 mpaka Tsh 90.9 bilioni, ikiwa imechangiwa na ongezeko la mikopo pamoja na mkazo katika amana zenye riba nafuu.

Aidha katika kipindi hicho hicho, mapato yatokanayo na tozo mbalimbali za huduma za kibenki yaliongezeka kwa asilimia 14 mpaka Tsh bilioni 35.7 ukilinganisha na Tsh bilioni 31.3 kwa mwaka uliopita. Ukuaji huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ufanisi kwenye utoaji huduma kwa wateja wakubwa na wale wa kati.

Faida hiyo imeongeza mtaji wa benki kufika Tsh bilioni 227 na kuongeza uwezo wa benki kuweza kufanya miamala ya kibiashara mikubwa zaidi.

Katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wateja na kujiandaa kwa ukuaji wa kasi, Benki ya Exim ametelekeza miradi mbalimbali ya kiteknolojia. “Nina furaha kubwa kuwataarifu kwamba kati ya miradi 8 ya kiteknolojia, miradi 7 imemalizika kwa mafanikio”. Alisema Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo Bw. Selemani Ponda na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia, benki itaweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake.

Utekelezaji wa miradi hiyo kwaajili ya kubadilisha mifumo ya kiutendaji umepelekea uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu na teknolojia na hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kupanda. Katika taarifa yake ya fedha jumla ya gharama ya uendeshaji ilipanda  kwa asilimia 24 hadi kufikia Tsh bilioni 99.

Benki ya Exim imejiandaa kuwahudumia wateja wa kada zote kutokana na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia wateja wote mara baada ya kutekeleza miradi ya kiteknolojia na kuongezeka kwa mtaji.

Akizungumzia mafanikio ya benki tanzu za Exim zilizopo katika nchi tatu: Komoro, Djibuti na Uganda, Bw. Ponda alisema kuwa Komoro na Djibuti wamefanya vizuri na kuweza kupata faida mara 3 ya mwaka uliopita na kufikia Tsh bilioni 8 kutokana na ukuaji mzuri wa uchumi na huduma bora. 

Na benki tanzu mpya ya Uganda ilipata hasara ndogo ya Tsh milioni 177, na inategemewa kufanya vizuri zaidi mwaka huu baada ya kuteleza mikakati mipya baada ya Benki ya Exim kununua hisa zaidi ya 58.6%.  

Chief Financial Officer of Exim Bank Tanzania, Mr Selemani Ponda as he shares with journalists that Exim Bank Group has achieved a pre-tax profit of TZS 83.6 Billion for the year 2016. The Group recorded a 25% growth in net interest income, fueled by asset book growth, better yields and reduction in cost of funds. Seated beside him are Senior Finance Manager, Joseph Mrawa [Left] and Deputy Finance Officer, Issa Hamisi [Right].

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...