Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao. 

Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja baada ya Kampuni ya Koberg Construction ya nchini hapa kuonyesha kusuasua na kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.

Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya maamuzi hayo baada ya kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo.

Kwa upande wake Katibu wa Bodi hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa 2014/2015 ndicho kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuamua kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na kumpatia wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...