Kituo cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao.
Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
 Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali  (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017  ukumbi wa Mayfair Plaza jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...