THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

CHADEMA YAPATA PIGO MUHEZA BAADA YA MWENYEKITI WA WILAYA KUJIUNGA NA CCM


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kwa kile anachodai kuwa  chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.

Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.
Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,  Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua  kujiunga na CCM ambako amesema kuna sera makini zinazotekelezeka.
Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.

“Kwa mfumo wa uongozi unaoongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia.... sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.

“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema na nitajiungha na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John Magufuli sababu Chadema wameacha sera na makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.

Alisema pia sababu nyengine ni kutokana na utendaji wa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambao umekuwa mstari wa mbelea kujali wanyonge na kusaidia harakati za kimaendeleo hapa nchini.

Aidha alisema wameshindwa kuelewa kuwa Mwenyekiti Mbowe alipangua gia angani kumuondoa dkta Slaa wakati alipokuwa kwenye chama hicho jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa chama hicho. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha akizungumza na waandishi wa habari mapema leo kutangaza azma ya kuondoka Chadema na kuhamia CCM