THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DAWASA YAKAMILISHA KAZI YA UPANUZI WA MTAMBO WA RUVU JUU: SASA WAZALISHA LITA MILIONI 196 ZA MAJI SAFI NA SALAMA

Baada ya kazi ya kuunganisha umeme wa kutosha kukamilika 15 Aprili, 2017 kazi ya kuwasha pampu kubwa mpya za majighafi na majisafi katika Mtambo wa Ruvu Juu sasa imekamilika rasmi ambapo mtambo huo sasa umeanza kuzalisha lita milioni 196 kwa siku. Taarifa ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar Es salaam (DAWASA) inaeleza.

Ili kufikia uwezo huo wa uzalishaji kutoka lita milioni 82 zilizokuwa zikizalishwa hapo awali, kazi mbalimbali zilifanyika ikiwemo ujenzi wa kituo kipya cha kusukuma maji na ufungaji wa pampu mpya, maeneo mapya ya kusafisha maji, mitambo ya kuchuja maji, maeneo ya kuchuja tope na tenki kubwa la kuhifadhia maji safi.

Katika kuhakikisha kuwa maji hayo yanawafikia wananachi, kituo kipya cha kusukuma maji safi na salama kilijengwa sambamba na mabomba makuu ya kusafirishia maji hayo yenye jumla ya urefu wa kilomita 70 kutoka Mlandizi hadi Dar es salaam.

Aidha, tenki jipya lenye uwezo wakuhifadhi lita milioni 10 limejengwa eneo la Kibamba lenye mwinuko; na kutoka hapo maji hushuka kwa nguvu ya mtiririko hadi katika matenki ya Kimara.

Kazi iliyokuwa imebaki ilikuwa ni kuongeza nguvu ya umeme ili kuwezesha pampu hizo mpya kufanya kazi. Hivi sasa kazi hiyo imekamilika, ukaguzi umefanyika na pampu moja baada ya nyingine zimewashwa ili kuhakiksha mfumo mzima sasa unafanya kazi.
Moja ya mitambo ya maji katika eneo la Ruvu Juu kama inavyoonekana, mitambo hii ni mipya na kwa sasa ndiyo itasaidia kuongeza uzalishaji wa maji toka lita milioni 82 hadi lita milioni 196 kwa siku.
Hii ni sehemu ya mtambo wa kusafirishia mai mara baada ya kusafishwa, hapa ndipo maji hukusanywa na kusafirishwa moja kwa moja kuelekea kwa wananchi.
Hii ni sehemu ya mtambo unaotumika kuwashia mitambo ya kusukuma maji katika eneo la Ruvu Juu.

Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Mtanzania Anasema:

    Hakika hii ni habari njema hasa kwa wananchi waliopo Kibamba na Ubungo, ifike sehemu sasa watu wapate maji bila mgao na hii itaongeza mapato na uwezo wa kulipa hili deni. Pia tuwafikishie maji wateja wengi zaidi. Taratibu tutafika