Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MKUU wa wilaya ya Mkuranga,mkoani Pwani, Filberto Sanga,ametoa mwezi mmoja kwa vyama vya ushirika vya msingi vya korosho(AMCOS), ambavyo vimehusika kufanya ubadhilifu wa fedha za korosho kwa wanunuzi,kuzirudisha ndani ya muda huo.

Amesema ameshakubaliana nao na wameahidi kuzirejesha kabla hajawachukulia hatua kali za kisheria. Sanga amechukua hatua hiyo kufuatia mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,kuvipa wiki mbili vyama hivyo ,kwenda kujieleza kwa wakuu wa zao ikiwemo Rufiji,Kibiti na Mkuranga .

Akizungumza na baadhi ya wananchi wilayani hapo katika kata ya Msonga,Njianne,kitomondo na Mwarusembe,alisema hujuma hizo hazivumiliki. Aidha Sanga, alisema mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo wenye tija kwa wakulima hivyo haupaswi kuchezewa. 

Alitoa rai kwa wakulima wa korosho kuacha kukubali kurubuniwa na madalali ama wanunuzi wachache hali inayosababisha kukosa mapato kulingana na korosho zao. Mkuu huyo wa wilaya ,alikemea tabia ya baadhi ya  watu wanaosafisha mashamba kwa kutumia kuchoma moto.

Alisema kitendo cha kuchoma moto mashamba kunaharibu mazingira ikiwemo kukata miti ovyo. Katika hatua nyingine, Sanga aliwaasa wananchi,kila familia kulima heka mbili za zao la mhogo. Alihimiza kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukomaa haraka ikiwemo mhogo, mtama, viazi vitamu na mikunde.

Sanga alieleza kwamba, akiwa na timu yake watapita kuhakiki kila familia kama imefuata agizo hilo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...