THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DIAMOND PLATNUMZ AZINDUA PAFYUM YAKE AINA YA (CHIBU), YAINGIA RASMI KWENYE SOKO, KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye amekuwa akifanya vyema ndani na anga za Kimataifa Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU,mapema leo jijini Dar.

Wakati wa uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza manukato 'pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi.

Amesema kuwa kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105, 000/-  kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi chupa ya Pafyum,mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Azori,wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia anafanya vyema katika kazi zake za Muziki,kushototo ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz almaarufu kwa jina la Babu Tale. 
 Msanii Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
 Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika jijini Dar Es Salaam mapema leo.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Diamond alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Pafyum hiyo ambayo tayari imekwisha sambaza kwenye maduka mengi jijini Dar.
Meneja wa Diamond Platnumz  Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana kwa jina la CHIBU.