Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WANANCHI wanaoishi vjijini hawana elimu ya uraia ya kuweza kujadili masuala mbalimbali yanayozunguka pamoja,namna ya kufatatilia taarifa zao kwa watoa huduma wa serikali.

Wakizungumza katika mkutano wa utoaji ripoti ya Mradi wa Elimu ya Uraia kwa Ujumbe wa Simu za Mikononi, wamesema kuwa mradi huo umesaidia wananchi kutatua changamoto zao kupitia kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu.

Akizungumza katika mkutano wa utoaji ripoti hiyo Mkurugenzi wa C-SEMA,Joel Kiiya amesema maeneo yaliyokuwa na changamoto kwa wananchi ni migogoro ya ardhi, Ndoa za Utotoni , Mimba za Utotoni , Miradhi pamoja na juu ya upatikanaji wa yeti vya kuzaliwa.Amesema mradi huo katika wilaya saba uliokuwa ukitekelezwa wananchi wamekuwa na elimu juu ya kupata huduma katika halmashauri .

Mrardi huo umetekezwa katika Wilaya za Karagwe, Chalinze, Bagamoyo , Shinyanga, Kyera, Kahama pamoja na Maswa.Mwakilishi wa Ofisi ya Rais , Katiba na Utawala Bora , Omary Hamis Juma , amesema kuwa Zanzibar walipokuwa wanatengeneza sera ya mtoto wamechukua sehemu ya C-SEMA kutokana vitu hivyo vitajenga katika sera hiyo.



Mkurugenzi wa C-SEMA, Joel Kiiya akizungumza katika Mkutano wa utoaji ripoti ya Mradi wa Elimu ya Uraia kwa Ujumbe wa Simu za Mikononi uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Ofisi ya Rais , Katiba na Utawala Bora-Zanzibar , Omary Hamis Juma akizungumza juu ya mradi ulivyoleta matokeo masula mbalimbali yanahusu jamii uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mwakili Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jaffari Malema akizungumza juu mradi katika matokeo watu kusajili vyeti vya kuzaliwa uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa C-SEMA, Itanisia Mbise akizungumza juu ya ukusanyaji wa ujumbe uliokuwa unatumwa katika maeneo ya mradi uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja washiriki wa mradi pamoja na maafisa wa serikali walioshiriki katika mradi huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...