NA HASSAN SILAYO.

Serikali imewataka watendaji serikalini kuzifanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na asasi za kiraia ili kuleta matokeo chanya na kuboresha maisha ya watanzania.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo wakati akipokea ripoti ya Takwimu Mpya za Uwezo Tanzania  iliyopo katika TWAWEZA.

Akiongea katika Hafla hiyo Naibu Waziri Jafo amesema kuwa Watendaji Serikalini sasa wana budi wa kufanyia kazi tafiti mbalimbali zinazotolewa na Azaki za kiraia zinazolenga  masuala yaliyopo katika jamii ili kuiwezesha serikali  kuyafanyia kazi matokeo ya tafiti na kuboresha hali ya watanzania.

“Kwa matokeo haya ya Tafiti ya TWAWEZA kupitia Uwezo Tanzania ni kipimo tosha cha kutuonesha sisi kama viongozi yapi tunayotakiwa kufanya na yapi hatutakiwi kufanya na yapi tunatakiwa tuyarekekebishe katika sekta ya elimu na matokeo haya tutayafanyia kazi”-Naibu Waziri Jafo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA Bw. Aidan Eyakuze akimkabidhi Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo matokeo ya Tafiti ya Uwezo Tanzania yaliyopo katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza? leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Seleman Jafo akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba matokeo ya Tafiti ya Uwezo Tanzania yaliyopo katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza? leo Mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakichangia mjadala mara baada ya kuwasilishwa kwa matokeo ya Tafiti ya Uwezo Tanzania yaliyopo katika ripoti ya Je, Watoto wetu wanajifunza? Ambapo walitoa mapendekezo kwa Serikali yenye lengo la kuboresha sekta ya elimu Nchini. PICHA NA HASSAN SILAYO.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...