THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

HALIMASHAURI YA MBARALI YATAKIWA KUWEKA MIFUGO YOTE CHAPA ILI KURAHISISHA UDHIBITI WAKE KATIKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Halimashauri ya Wilaya ya Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng’ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa chapa ili kurahisisha kuweza kujua ng’ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia kila mfugaji awe na ng’ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia uharibifu wa mazingira uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi. 

Katika maagizo hayo pia Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa kushirikiana na Wananchi wake kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na kuingizwa kwa mifugo katika mto Ndembela kwa ajili ya kunywa maji.

Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea na Wananchi wa kata ya Madibira wakati wa mkutano na Wananchi juu ya kujua na kufahamu changamoto mbalimbali zinazosababaisha uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito inayozunguka Mto wa Ruaha Mkuu ukiwemo mto Ndembela.

Akiongea katika Mkutano huo Bwana Muyungi pia ameahaidi kushughulikia Wawekezaji ambao siyo waaminifu wanaotumia maji bila kibali cha Serikali au wale ambao wanazidisha kiwango cha uchukuaji maji tofauti na kile kilichoanishwa katika kibali . Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu na kuhakikisha rasilimali zote zilizopo Nchini zinatumika kwa usahihi .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha pamoja na Wananchi wa Kata ya Madibira wilayani Mbarali Mkoani Mbeya. 
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.