Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
imepongeza na kutoa zawadi kwa shule kumi za Msingi na moja Sekondari kwa kufanya vizuri kwenye
mitihani ya darasa la saba na kidato cha
nne mwaka 2016. Zawadi hizo zilitolewa kwenye kilele cha maadhimisho ya juma la
elimu yaliyofanyika kiwilaya Wilayani Handeni kwenye shule ya Msingi Kabuku
nje.
Akizungumza kwenye maadhimisho
hayo Mkuu wa Wilaya ya Handeni ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Mh. Godwin
Gondwe aliwapongeza walimu na wadau wengine wa elimu kwa kazi nzuri wanazofanya
na wanazoendelea kufanya katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
“elimu ni ufunguo wa maisha na
kwamba Handeni hakuna mtoto mjinga, wazazi na walezi himizeni watoto kutumia fursa ya Elimu bure
inayotolewa na Raisi wa Tanzania” Alisema.
Aidha ameeleza kuwa atahakikisha
fedha zinazohusu madai ya walimu
zinapofika Halmashauri zinawafikia
walengwa kwa wakati uliopangwa. Aliwataka wakuu wa shule na Maafisa elimu Kata
kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.
Wakati huohuo amepiga marufuku
watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuacha kuchunga mifugo hasa kwa siku za
shule baada ya kubainika watoto wengi wa jamii ya wafugaji wanatumiwa kuchunga
mifugo badala ya kwenda shule.
Amewaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao
wanakwamisha watoto kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria
itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume. Amewaeleza pia wazazi
ambao wanawatoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akikabidhi zawadi kwa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Tewe iliyokuwa ya kwanza kiwilaya na ya sita kimkoa
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe wakisomewa namba na wanafunzi wa shule ya awali kabuku nje
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe na Mkurugenzi Mtendaji wakisikiliza mwanafunzi alipokuwa akielezea tense za somo la kiingereza
wanafunzi wa shule ya sekondari kabuku akielezea mifumo ya kibaiolojia Kwa viongozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...