THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JE WEWE NI MIONGONI MWA WALIOSUBIRIA MWEZI APRILI KWA HAMU?


Na Jumia Travel Tanzania

Kama kuna kitu ambacho wafanyakazi wengi wanapenda kusikia basi ni sikukuu au mapumziko. Kwani hupata fursa ya kutokwenda kazini, haimaanishi kwamba ni wavivu bali kutokana na ufinyu wa likizo ukiachana na wikendi.
Kwa upande wa watanzania hali hiyo hutokea kwa baadhi ya miezi na wa Aprili ni mmojawapo. Kutokana na utafiti mdogo uliofanywa na Jumia Travel, zifuatazo ni sababu zinazoufanya mwezi huu kupendwa zaidi nchini.
Sikukuu ya Karume. 
Hii siku huadhimishwa kila ifikikapo April 7 ya kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kuuawa kwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa visiwa vya Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume mwaka 1972 katika eneo la Mji Mkongwe, Unguja. 


Hivyo basi kama taifa huiadhimisha siku hiyo kwa wananchi kupumzika na kutofanya shughuli yoyote na badala yake kumkumbuka shujaa huyo aliyeongoza mapinduzi dhidi ya waarabu waliokuwa wakivikalia visiwa hivyo kwa mabavu. Kwa mwaka huu ni tofauti kidogo kwani siku hiyo itaangukia Ijumaa na hivyo kutoa fursa kwa watu kupumzika kwa siku tatu ukijumuisha na wikendi. Kwa wenye mipango mifupi kwenye mapumziko hayo wanaweza kutekeleza azma zao, kama vile kusafiri nje kidogo ya mji. 

Sikukuu ya Pasaka. 
Kwa wakristo wengi nchini Tanzania na duniani kote kwa sasa wapo kwenye mfungo wa Kwaresma ambao ulianza tarehe mosi ya mwezi Machi na kudumu kwa siku 40. Kwa mujibu wa kalenda mfungo huo utaisha siku ya Alhamisi ya tarehe 13 ya mwezi Aprili. Maandalizi ya sikukuu ya Pasaka huanza siku ya Ijumaa Kuu, tarehe 14, ambayo ni siku ya mapumziko huku sikukuu yenyewe ya Pasaka itakuwa ni Jumapili ya tarehe 16. Lakini haiishii hapo kwani shamrashamra za Pasaka zitaendelea mpaka siku ya Jumatatu ya tarehe 17. Hivyo, kwa haraka haraka watu watakuwa na mapumziko ya siku nne mfululizo na ndio maana husubiriwa kwa hamu kubwa huku kukiwa na mipango lukuki ndani yake. 


Tembelea Jumia Travel kujua sehemu zilizo karibu nawe ambazo unaweza kwenda na kufurahia kwa siku hizo chache pamoja na wapendwa wako.

Sikukuu ya Muungano. 
Ifikapo tarehe 26 ya mwezi wa Aprili pia watanzania watakuwa na sherehe nyingine muhimu katika historia ya taifa lao. Siku hiyo inakumbukwa kwa Tanganyika kuungana na visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba) mnamo mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ilivyo ada siku hii nayo ni mapumziko kwa watanzania wote, watu hawaendi kazini na badala yake kusherehekea siku hiyo kwa kuutafakari umuhimu wa Muunganao na faida zake kwa wananchi wa pande zote mbili kwa pamoja.