THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KAGERA WAZITAKA POINTI ZAO ZIRUDISHWE, WATUMA BARUA TFF

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Soka ya Kagera imeaiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

Braua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo  Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.

Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka jana usiku naada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya  alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.

Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.

Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

Baaada ya maamuzi hayo Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Mohamed Msami Anasema:

    Kama tunataka kuipa timu ubingwa ili hali haina uwezo ushindi wake ni kwa kutumia hongo tunajiangusha wenyewe ndio maana hata Fifa ilibidi viongozi wa juu waondolewe kwa kashfa za rushwa Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na mpira wetu bila kuweka mbele utimu kilichofanyika sio haki na mwenyezi mungu awalaani hao wa watu wa saa 72 kwa kuchukue hongo kupindisha sheria.