Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Soka ya Kagera imeaiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

Braua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo  Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.

Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka jana usiku naada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya  alitoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.

Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.

Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba. Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

Baaada ya maamuzi hayo Simba wamejikita kileleni zaidi wakiwa na alama 61 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 56.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kama tunataka kuipa timu ubingwa ili hali haina uwezo ushindi wake ni kwa kutumia hongo tunajiangusha wenyewe ndio maana hata Fifa ilibidi viongozi wa juu waondolewe kwa kashfa za rushwa Watanzania wenzangu wenye mapenzi mema na mpira wetu bila kuweka mbele utimu kilichofanyika sio haki na mwenyezi mungu awalaani hao wa watu wa saa 72 kwa kuchukue hongo kupindisha sheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...