Kampuni tanzu ya chakula na vinywaji nchini, imezindua bidhaa yenye mchanganyiko wa kahawa, maziwa na sukari ya “Nuru coffee Chapchap” yenye hadhi ya kimataifa na ladha thabiti. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Rayton Kwembe amesema kampuni hiyo imewawezesha Watanzania hata ya hali ya chini, kuwa na uwezo wa kuonja ladha murua yenye mchanganyiko wa maziwa, sukari na kahawa kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh 500=/

“ Nuru coffee Chapchap ni bidhaa ya kipekee na ni moja kati ya bidhaa madhubuti katika kampuni yetu. Nuru ni neno la Kiswahili linamaanisha “mwangaza” ikiwa na maana ya asili, Nishati, na matumaini . Nuru huondoa giza na kuweka dhahiri vitu vilivyofichika. Nuru hung’aa popote na kurudisha tumaini kwa watu waliokata tamaa.”

Amesema uzinduzi wa kahawa ya Nuru coffee Chapchap imekuja kwa wakati muafaka na kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa za ajira zinazotolewa nchini na kampuni hii na pia bidhaa ya nuru coffe imekuwa nuru kwa watanzania kwani imewawezesha kujipatia chai yenye mchanganyiko wa sukari maziwa na kahawa kwa gharama nafuu kabisa kwa kuzingatia hali yetu uchumi.

“Tunayofuraha kubwa kuzindua bidhaa hii ya kiwango cha juu itakayokidhi maisha ya mtumiaji, kwa kumpatia ladha nzuri ya kahawa bora kabisa na chapchap. Nuru coffee Chapchap inatokana na aina mbili kuu za kahawa nchini, Robusta na Arabika kwa asilimia 100 na kutengenezwa kwa mchanganyiko madhubuti wa maziwa na sukari, ili kuleta ladha nzuri ya kuvutia. Tumejipanga na tuna ujasiri mkubwa juu ya bidhaa yetu mpya na hivyo hatutatetereka.”

Kwembe amesema sasa Nuru coffee Chapchap inapatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Mbeya, Dodoma na Arusha, na pia bidhaa hii inatarajiwa kupatikana mikoa mingine nchini miezi michache baadae.

Katika kusherekea uzinduzi wa Nuru Coffee Chapchap katika soko la nchini Tanzania kampuni ya DMG Tanzania imeandaa kampeni itakayohusisha supamaketi kubwa mbalimbali kama TSN Supermarkert iliyopo kibo complex, American Super Markert pugu road na Nakumatt Mlimani City. Kampeni hiyo pia itahusisha upatikanaji wa nuru Coffee katika mitaa mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 – 25 Aprili mwaka huu.

Kitu kikubwa Zaidi katika bidhaa ya Nuru coffe ni utaalamu wa usindikaji wa bidhaaa hiyo na ufungaji wa paketi zake zinazolenga kuibua hisia ya mtumiaji kabla hata hajainunua.
 Balozi wa Kinywaji cha Kahawa , Msanii wa  Bongo Flava, (G Nako) George Mdemu akizungunza wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho jijini Dar es Salaam.
 
Sehemu ya wananachi wakionja kahawa iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...