UJIO wa Kocha Sue Purchase kutoka katika shule ya kimataifa ya Mtakatifu Felix Uingereza kusaka vipaji vya mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya taifa kutawanufaisha wachezaji watakaoonyesha uwezo. Mashindano ya klabu bingwa Taifa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii na kushirikisha wachezaji 172 kutoka klabu 15 za Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA) Ramadhan Namkoveka, Purchase ambaye pia  ni Mkurugenzi wa michezo wa kuogelea wa shule hiyo, atahudhuria mashindano hayo dhamira  yake kuu ni kusaka vipaji vya mchezo huo. Alisema kuwa hatua ya Purchase kuja nchini imetokana na uwezo mkubwa wa waogeleaji wa Tanzania wanaosoma katika shule hiyo kwa njia ya ‘scholarship’, ambao ni Sonia Tumiotto, Collins Saliboko, Anjani Taylor,  Smriti Gokarn na Aliasgar Karimjee.

“Wachezaji hawa ambao wanasoma uingereza tayari wameshawasili hapa nchini hivi karibuni tayari kushiriki mashindano ya Taifa na wanaendelea na mazoezi ya mwisho hapa Dar es Salaam,”alisema.

Namkoveka alisema kuwa waogeleaji wameonyesha viwango vya hali ya juu kiasi cha kumfanya Purchase kuamua kufunga safari ya kuja nchini kushuhudia waogeleaji wengine wa Tanzania ili kujionea mwenyewe katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Davis & Shirtliff, CRDB Bank, Mediterraneo Hotel & Restaurant, Cocacola na The Terrace.

“Tunawashaukuru makampuni haya kuweza kutisaidia, kwa hakika mchango wao utasaidia kuinua mchezo wa kuogelea. Tunaomba ushirikiano huu uendelee kwa maslahi ya mchezo wa kuogelea na michezo hapa nchini,”alisema. Alisema kuwa mbali ya kushuhudia mashindano hayo na kusaka vipaji, kocha huyo atakutana pia na wazazi na, makocha, waogeleaji wa klabu ya Dar Swim Club na kufanya  nao mazungumzo.

Alisema kuwa hii ni faraja kwa wadau, wachezaji, vilabu  na viongozi wa mchezo wa kuogelea kwani ujio wa kocha huyo ni ishara ya mchezo kukua. Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya klabu 15 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambazo zitashindana katika staili za backstroke, freestyle, breaststrokes, Butterfly na Individual Medley (IM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...