THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KUMBUKUMBU YA DKT. AARON DAUDI CHIDUO


Tarehe 23 May 1933 – 13 April 2007

Baba yetu mpendwa, Masaa, Siku, Wiki, Miezi na sasa ni miaka 10 tangu Mungu wetu mwenye wingi wa rehema na upendo alipodhihirisha utukufu na mapenzi yake makubwa kwako hadi akaamua kukuchukua alfajiri ya siku ya Ijumaa terehe 13/04/2007. 

Huzuni na majonzi bado vimebaki kuwa ni sehemu ya maisha yetu katika familia lakini tunalo lile tumaini la Neno la Mungu kuwa siku moja tutaufikia ule ufufuo wa milele ndani ya Kristo pamoja. Matendo yako mema yamebaki kuwa lulu na mwanga uiangaziayo familia yetu. Maisha yako ya upendo, unyenyekevu, uadilifu, utu wema na bidii katika kazi ndiyo dira inayotuongoza: mke wako Mama Ahilai, watoto wako Sydney, Sarah, Oripa, Geoffrey, Rodney, wakwe zako Pascal, Joel, Eunice na Salome pamoja na wajukuu zako Dennis, Karen, David, Samantha, Jovin na Daniel. Tutakukumbuka siku zote kwa kukukosa katika mengi.

Dada zako, kaka zako na familia zao na ndugu wengine wote wa koo za Chiduo, Chitemo, Chigongo, Mheta, na Msele nao pia wanakukumbuka sana. Kwetu sote imebaki kumbukumbu ni jinsi gani ulikuwa mhimili wa familia na ukoo mzima kwa ujumla.

Baba, kwako tulijifunza uaminifu, uadilifu, unyenyekevu na kupenda haki vitu ambayo viliyokujengea heshima kubwa miongoni mwa jamii.
Mchango wako mkubwa ulioutoa katika kulitumikia Taifa hili utakumbukwa siku zote na wachapa kazi wote.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.

1 Wathesalonike 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu


13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake.