Dar Running Club ikishirikiana na Kampuni ya maji ya kunywa Dasani,
leo imeanza kufanya usajili kwa washiriki
wa mbio za km 10 na 21km zijulikanazo kama Dasani Marathoni
zitakazofanyika Jumapili ya Mei 14, 2017
jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Dar Running Club kuendelea kuihamasisha
jamii kufanya mazoezi kwa kuandaa mashindano haya, ambayo yatafanyika
tarehe Jumapili ya Aprili
2017. Awali mashindano haya yalikuwa yakijulikana kama May Day Marathon
lakini kutokana na kushirikiana na kampuni ya maji ya Dasani kuyaandaa mwaka
huu yatajulikana kama Dasani Marathon 2017.
Akizungumzia
mashindano haya, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza LTD, kampuni
ya inayotengeneza maji ya Dasani, Nalaka Hettiarachchi amesema kuwa maji ya kunywa
ya Dasani ni murua na yenye kuondoa kiu, hususani wakati wa kufanya mazoezi au
unapojisikia kuburudika na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwa
wingi ili kujenga afya zao kwa mazoezi.
Pia akiamini kuwa tunaweza kuleta
uzoefu mkubwa kwa wahsiriki na kulifanya kuwa tamasha la kukumbukwa. Pia
tutalifanya tukio hili kuwa maarufu zaidi na lakusisimua kwa miaka ijayo likiwa
na vivutio vingi kwa washiriki kutoka katika matembezi mbali mbali”. Lengo letu
kubwa ni kusaidia vijana na kuhamasisha Watanzania wenye vipaji kufikia viwango
vya Kimataifa and kuleta heshima kwa nchi yako… aliongeza Nalaka
Kwa upande wake, rais wa Dar
Running Club, Goodluck Elvis, alisema
kauli mbiu ya klabu yao ni "Active. Wherever. Whenever" na imefarijika kuungana na Dasani katika kuandaa
mashindano haya Dasani Marathon 2017 ambayo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka
kwa kasi mwaka hadi mwaka.
Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka miwili iliyopita, mbio hizo
zitaanzia na kumalizikia Police Officers
Mess Oysterbay. Mbio za 21km zitaanza saa kumi na mbili kamili alfajiri,
zikifuatiwa na zile za 10km ambazo zitaanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi.
Washindi watano wa mbio za 21km na washindi watatu wa mbio za 10km watazawadiwa
zawadi nono ikiwemo fedha taslimu.
Kiwango cha kusajili ni TZS 30,000/= kwa mbio zote na mwisho wa
usajili ni tarehe 13 Mei, 2017.
Vituo vya awali vya usajili vitakuwa
Colosseum Gym - Masaki, Shoppers plaza – Mikocheni, China Plaza: Ghorofa
ya 11 mtaa wa Uhuru na Mheza Kariakoo na Mlimani City Mall. Washiriki wote
watafanikiwa kupata fulana zenye kiwango cha juu na vilevile watazawadiwa
medali pindi watakapokamilisha mbio hizo kwa wakimbiaji elfu moja wa kwanza.
Kwa
Taarifa Zaidi wasiliana na:
Goodluck Elvis, Dar Running Club – President,
0715 302 336
Erick Kahwa, Dar Running Club – Secretary,
0784024422
Dorothy Kipeja, Dasani Marathon Marketing Manager – 0754 291
291
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...