THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAZIDI KUIVA UWANJA WA UHURU,PIA KUFANYIKA MIKOA YA MWANZA NA SIMIYUMkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni,jijini Dar es salaam kuhusiana na  maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 16 kwenye uwanja wa Uhuru na kutumbuizwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa mbalimbali na nchini Tanzania.

Msama amesema mwimbaji nguli kutoka nchini Afrika ya Kusini Solly Mahlangu atakuwa ni mmojawapo wa waimbaji kutoka nje ya nchi wakiwemo wengine kutoka nchini Kenya, Ameongeza kuwa tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa ya Mwanza na Simiyu, hata hivyo tamasha hilo halitafanyika katika mkoa wa Dodoma kama ilivyotangazwa awali kutokana na uwanja wa Jamhuri ambao ulikuwa utumike siku hiyo kuwa na shughuli nyingeni. 
Msama amesema kuwa katika tamasha hilo la Pasaka litakalofanyika katika Uwanja wa Uhuru,Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh.Mwigulu Nchemba,baada ya tamasha hilo kurindima jijini Dar litahamia Simiyu na jijini Mwanza ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula .
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Bw. Alex Msama katika mkutano huo.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama alipokuwa akisisitiza jambo kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka