THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA KUWASAFIRISHA WATANZANIA WATATU KWENDA MAREKANI KUSIKILIZA TUHUMA ZINAZOWAKABILI

Na Karama Kenyunko

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali maombi ya Waziri wa Katiba na Sheria ya kuwasafirisha watanzania watatu  wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwenda nchini Marekani kusikiliza tuhuma zinazowakabili.

Hakimu Mkazi mfawishi Cyprian Mkeha ametoa uamuzi huo leo. Wajibu maombi hao ni Ally Hatibu Hassan maarufu kama Shkuba, Iddi Salehe Mafuru, na Lwitiko Emmanuel Adam.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Mkeha amesema, wajibu maombi hao watakaa rumande hadi kibali kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria kitakapotolewa. Aidha mahakama imesema kuwa wajibu maombi wanahaki ya kukata rufaa ndani ya siku 15 kabla ya Waziri wa katiba na Sheria hajatoa Kibali cha  kuwasafirisha.

Mapema wiki hii Waziri wa Katiba na Sheria  kupitia Wakili Mkuu wa Serikali Edwin Kakolaki aliwasilisha maombi ya kuwasafirisha wajibu maombi hao kwenda nchini humo kujibu tuhuma za kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya.

Katika maombi hayo, wajibu maombi wanadaiwa kuhusika kwenye njama za kusafirisha na kusambaza zaidi ya kilo moja ya Heroine nchini humo.