Na Bashir Yakub.
Yapo mambo unayotakiwa kufanya mara tu baada ya kusajili kampuni. Tunazungumzia yale utakayoyafanya ule mda baada ya kuwa umepewa cheti cha kuzaliwa kwa kampuni( certificate of incorporation) kutoka BRELA. Mambo haya ni ya kisheria na kutoyafanya kwake kunahesabika ni kuvunja sheria. Kwahiyo mambo haya ni lazima na sio hiari.
Hata hivyo kabla ya kueleza hayo ni muhimu tukajikumbusha kuhusu taratibu za kusajili kampuni. Tunasema kujikumbusha kwakuwa makala kuhusu taratibu na namna ya kusajili/kuunda kampuni hatua kwa hatua yalishaandikwa hapo awali. Haya yote yatakuwa yakitoka Sheria ya Makampuni ,Namba 12 ya mwaka 2002.
1.HATUA ZA KUSAJILI/KUUNDA KAMPUNI.
( a ) Kwanza hakikisha unajua unahitaji kufanya biashara gani. Hii ni kwasababu katika vitabu vya kampuni lazima uandike biashara unayotaka kufanya au unayofanya tayari.
( b ) Hakikisha mko wawili au zaidi. Hakuna kampuni ya mtu mmoja. Kampuni binafsi huanzia watu wawili na mwisho ni watu 50. Unaweza kuwa wewe na mke wako, rafiki, ndugu, mzazi, mtoto nk.
( c ) Fahamu kampuni yenu inatakiwa kuwa na hisa ngapi na kila hisa itakuwa inauzwa bei gani. Pia unatakiwa kujua kampuni itakuwa na mtaji wa shilingi ngapi. Kwa mfano kampuni itakuwa na hisa 10000, bei ya kila hisa ni Tshs 1000 ambapo, hisa x bei ya hisa = mtaji wa kampuni, kwa maana ya 10000 x 1000 = 10000000 ambao ndio mtaji wa kampuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...