Na
Bashir Yakub
Ni kipindi muhimu
kujua kuhusu hisa. Hivi
karibuni utakuwa umesikia
makampuni mbalimbali hasa
yale ya simu
yakiwatangazia watu kununua
hisa. Ni muhimu kwako
kujua kuhusu biashara
hii. Huenda ikawa
ya faida kwako
au eneo zuri kwako
kwa kuwekeza.
Mapema niseme kuwa
usiogope wala usiwe mwenye hofu. Biashara ya
hisa ni ya
watu wote tajiri au
maskini. Laki moja,
laki mbili nk. unaweza
kununua hisa. Ili umiliki
hisa kwenye kampuni ya simu
si lazima umiliki
mamilioni kama unavyodhani.
Na hapa ndipo
tunapokosea na kuwaacha matajiri
watambe nasi tubaki
kulalamika.
1.HISA NI NINI.
Hisa ni mali
kama zilivyo mali
nyingine unazomiliki.
Tofauti ya hisa
na mali nyingine ulizonazo kama
shamba, gari, nyumba
nk.ni kuwa mali
nyingine huweza kushikika
au kuonekana kwa
macho wakati hisa
ni mali isiyoonekana
kwa macho. Yumkini
zote ni mali
tu.
Hisa ni maslahi
au haki fulani
unayokuwa nayo katika taasisi au
kampuni fulani. Ndiyo
maana ni mali
isiyoonekana kwasababu huwezi
kuona maslahi au
haki kwa macho.
2. KUMILIKI
HISA KATIKA KAMPUNI.
Kampuni yoyote unayoiona huwa inao
wanahisa. Wanahisa ndio
wamiliki wa kampuni.
Kwahiyo hata wewe
ukinunua hisa kwenye
kampuni yoyote na
wewe unakuwa mmoja
wa wamiliki.
Haijalishi ukubwa wa kampuni
na kiwango chako cha
hisa ulichonunua bali ni
kuwa ukishanunua tu
hapohapo na wewe
unakuwa mmoja wa
wamiliki. Hata hisa za
laki moja nazo
zinakufanya kuwa mmoja wa
wamiliki.
Kiwango cha hisa zako
ndicho kiwango cha
umiliki wako. Kampuni
ikiwa na hisa
100,000 na wewe
ukamiliki hisa 50,000 basi
wewe unaimiliki nusu
ya kampuni. Ukimiliki
hisa 25,000 basi
wewe unamiliki robo
ya kampuni. Halikadhalika
ukimiliki hisa 500,
100, 50, 10, 5
au hata hisa
3 basi hichohicho
kiwango chako cha hisa
ulichonunua ndicho kiwango
chako cha umiliki wa
kampuni husika.
Kwahiyo ukinunua hisa
100 Vodacom basi
wewe utaimiliki Vodacom
kwa kiwango cha hisa hizo
ulizonunua. Isipokuwa ni muhimu
kujua kuwa anayemiliki
hisa nyingi kuliko wote
ndiye hujulikana kama
mmiliki mkuu wa
kampuni.
3. JE
UTAFAIDIKAJE NA HISA.
Kila mwanahisa hupata
gawio la faida
pale kampuni inapotangaza
faida. Kampuni hutangaza
faida kila baada
ya mwaka au
nusu mwaka au vinginevyo.
Utapata mgao
kwa asilimia kutokana
na kiwango chako
cha hisa ulizonazo. Ukiwa na
hisa nyingi utapata mgao
mkubwa, ukiwa na
hisa kidogo utapata
mgao mdogo na
vivyo hivyo.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...