Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

Amesema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

Aidha, Makamba amewataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.

Vile vile, ameongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

"Hali hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,"amesema Makamba.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.​
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mheshimiwa January Makamba  akizungumza na Waandishi wa habari ofsini kwake mapema leo juu ziara ya Makamu wa Rais nchini Mama Samia Suluhu Hassan katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kushoto Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo Bw. Richard Muyungi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  juu ya athari za kuchepusha mto
 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakimskiliza waziri makamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...