Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua Kikosi Kazi Maalum kwa ajili ya kuokoa mfumo wa ikolojia katika bonde la mto Ruaha Mkuu ambalo lipo katika hatari ya kutoweka kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea kwenye bonde hilo kutokana na shughuli za Kibinadamu.

Kikosi kazi hicho ambacho kimezinduliwa mjini Iringa kitafanya kazi chini ya usimamizi wa Makatibu Tawala wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe kwa kuchambua kwa kina tafiti na matokeo ya tafiti hizo ili kupendekeza hatua za haraka zitakazochukuliwa katika kudhibiti uharibifu kwenye bonde hilo ambao umechangia kupungua kwa maji kwenye mto Ruaha Mkuu.

Akizindua Kikosi kazi hicho mjini Iringa ambacho ambacho kimehudhuriwa na Mawaziri kutoka Wizara Tano, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ofisi yake imeamua kuunda kikosi hizo ili kuokoa hali mbaya ya uharibifu wa mazingira unaoendelea kufanyika hivi sasa katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.

Amesema kutokana hali kuwa tete kwenye bonde hilo ndio maana hatua ya haraka na za dharura zimechukuliwa na ofisi yake kwa kuunda kikosi kazi hicho ambacho kinaundwa na wataalamu mbalimbali wa serikali, washirika wa maendeleo ambao wana uwezo wa kufanya maamuzi ya kisera na kiutendaji ili kutoa suluhu ya kudumu ya kuhifadhi bonde hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiongoza mkutano wa uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa. 
Mhe. January Makamba akithutubia juu ya umuhimu wa mto Ruaha ambao unahudumia watu zaidi ya milioni 6 na namna ambavyo umeathirika na shughuli za binadamu kwenye warsha ya uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo- ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MB) Mhe. Wiliam Lukuvi (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina  Masenza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kikosi kazi cha kuokoa mfumo-ikolojia wa bonde la mto Ruaha Mkuu uliofayika kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.



Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Mhandisi Gerson Lwenge akihutubia wakati wa warsha ya uzinduzi wa kikosi kazi cha kokoa mfumo -ikolojia wa bonde la mto Ruaha mkuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...