THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAMA MAGUFULI ASHIRIKI KATIKA HAFLA YA KUMUAGA PAROKO WA PAROKIA YA OYSTERBAY FR. STEPHANO KAOMBWE ANAYEHAMIA CHANG'OMBE

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli  Jumapili  April 2, 2017 ameungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya  Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia  Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke.
Kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rigambwa  wa Kanisa la Mtakatifu Petro na kuongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mama Magufuli amemtakia kila la heri Fr. Kaombwe katika kituo chake kipya cha kazi, na pia amempa salamu toka kwa Rais John Pombe Magufuli ambaye naye amemtakia heri na fanaka kwa uhamisho huo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa alimpongeza Fr. Kaombwe kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati akihudumu katika Paroko hiyo kwa takriban miaka mitatu na nusu, na pia alitumia nafasi hiyo kumtambulisha Fr. Asis Sylvester Mendoca ambaye atakaimu nafasi ya Fr. Kaombwe.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, amempongeza Fr. Kaombwe kwa mambo mengi aliyoyafanya kanisani hapo, na kwa niaba ya jumuiya ametoa shukurani nyingi kwa huduma alizokuwa akiwapatia.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiongea machache alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro  jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia  Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru (kushoto) na Fr. Asis Sylvester Mendoca (wa pili kulia) wakimsikiliza Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Kanisa la Chang’ombe, wilayani Temeke, akiongea kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa akiongoza sala wakati wa hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe (kulia), Paroko aliyekuwa anahudumu katika  Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe. Kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli. Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na masista alipoungana na waumini, ndugu jamaa na marafiki kumuaga Fr. Stephano Kaombwe,, Paroko aliyekuwa anahudumu katika Parokia ya Oysterbay katika Kanisa la Mtakatifu Petro  jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika picha ya pamoja na waumini, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam Mhashamu Eusebius A. Nzigilwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walei wa kanisa la Mtakatifu Petro, Dkt. Adelhem Meru, Fr. Asis Sylvester Mendoca baada ya kuhitimisha hafla ya kumuaga Fr. Stephano Kaombwe, Paroko aliyekuwa anahudumu Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam, ambaye sasa anahamia Parokia ya Chang’ombe, wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa.