THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

YANGA YAICHAPA MC ALGER 1-0 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiwania mpira na Beki wa MC Alger ya nchini Algeria, Hachoud Abdullman, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda kwa  bao 1-0 lililowekwa kimyani na Thaban Kamusoko.


Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya hatua ya mtoano ya kombe la Shirikisho Yanga wamefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria.
Mchezo huo uliopigwa leo majira ya saa 10 Alasiri katika dimba la Uwanja wa Taifa ukichezeshwa na mwamuzi kutoka Burundi Louis Hazikumana.

Kipindi cha kwanza kilianza kwa Kila upande kusaka goli la kuongoza lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Mzambia Obrey Chirwa ilishindwa kutumia nafasi walizozipata.
Mpaka mapumziko timu zinaingia vyumbani, matokeo yalikuwa ni 0-0. Kipindi cha pili kilianza kwa MC Alger kulisakama lango la Yanga lakini umakini wa safu ya ulinzi ilikuwa makini na kuondosha hatari langoni mwao.
Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko ya kwanza na kumtoa Deus Kaseke ambapo mabadiliko hayo yanaleta tija na katoka dakika ya 61 Thaban Kamosoku anaipatia Yanga goli la kwanza.
Yanga walianza kubadilika na kuendelea kulisakama goli la MC Alger lakini Chirwa anakosa umakini na kukosa magoli ya wazi.
Baada ya matokeo hayo, mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa April 15 nchini Algeria ambaoo Yanga inatakiwa kuhakikisha wanatoka na ushindi au sare ya aina yoyote ili kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Obrey Chirwa akiongoka na mpira mbele ya Mabeki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
 Wachezaji wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria wakimdhibiti Mshambuliaji wa pembeni wa Timu Yanga, Hassan Kessy, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
 Mchezaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akijirabu kuchukua mpira mguuni mwa Beki wa Timu ya MC Alger ya nchini Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, unaochezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.