THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MC ALGER KUTUA ALHAMIS USIKU, YANGA YAJIZATITI KUBAKISHA USHINDI NYUMBANI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Wapinzani wa Yanga katika mtuano ya kombe la Shirikisho badani Afrika kutoka nchini Algeria, MC Alger wanatarajiwa kuingia nchini siku ya Alhamis wakiwa na msafara wa watu 40 .

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio huo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa wametumiwa taarifa kuwa timu hiyo itawasili majira ya saa 3 usiku kutoka nchini Algeria.

Mkwasa amesema kuwa, kuelekea mchezo huo utakaochezwa Jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa utakuwa wa ushindani mkubwa sana kwani wanazifahamu vizuri timu za kiarabu.

Amesema kuelekea mchezo huo kwa sasa benchi la ufundi linaendelea kuwapa wachezaji mbinu mbalimbali na tayari wameshaanza mazoezi na wameingia kambini kwa ajili ya kupata umakini zaidi." timu yetu kwa sasa inaongoza ligi na tupo katika njia nzuri za kuutetea ubingwa wetu. Hawa wanaoleta maneno ya uzushi hawana nia njema na klabu , wanataka watu waache kufanya kazi ili malengo yao yatimie . Klabu haipo katika mpango ambao moja kwa moja ni hasara kwa klabu kuanza kulipa fidia na kupoteza malengo yake ,"amesema Mkwasa.


Amevitaja viingilio vya mchezo huo wa kimataifa wa hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho Afrika kima cha chini ni 5000 , VIP B & C 20000 na VIP A ni 30000.

Mkwasa amewaomba mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yao siku ya Jumamosi ili kuipa sapoti timu yao pendwa.


" tunahitaji kushinda hapa nyumbani ili kupunguza ugumu wa mechi ya ugenini , hivyo sapoti yenu itakuwa ni msingi mzuri wa morali kwa vijana,"amesema Mkwasa.         
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya MC Alger ya Algeria wa hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho.