THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mdahalo Maalum: Watanzania Wa Nyumbani Na Diaspora Kukutanishwa

Ni Jumanne na Jumatano, Aprili 11 na 12. Ni mdahalo kuhusu nafasi ya Diaspora kuungana na wenzao walio nyumbani kwenye kuchangia kusukuma mbele jitihada za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda kutokana na maendeleo ya viwanda. 
Hivyo, umuhimu wa kujadili fursa na changamoto.Tukio hilo ambalo ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka Kumi ya kuanzishwa kwa mtandao wa ' Mjengwablog' litafanyika Aprili 11 na 12 ( Jumanne na Jumatano) kwenye Ukumbi wa Nyumba ya Makumbusho, Dar Es Salaam. 
Ukumbi upo Mtaa wa Shabaan Robert na utazamana na IFM.Mdahalo utaambatana na maonyesho ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania na wajasiriamali wa Kitanzania. Washiriki wa mdahalo huo wanaotarajiwa kuwa zaidi ya mia mbili wanatazamiwa kuwa katika makundi matatu makuu; Baadhi ya Watanzania waishio ughaibuni, waliokuwa wakiishi ughaibuni na sasa wamerejea nyumbani na Watanzania wa nyumbani. Wote hao wanaunganishwa jambo kuu lenye kuhusu maendeleo ya uchumi wa nchi na kwa ngazi ya mtu binafsi. Hivyo, inahusu kujadili fursa za kufanya biashara na uwekezaji. Mdahalo hauna kiingilio.
Na Alhamisi April 13, kutakuwa na ' Usiku wa Nyumbani Na Diaspora' kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama. Kutakuwa na chakula cha Kiafrika na maonyesho ya mavazi ya Kiafrika. Baada ya hapo ni mwendo wa kujirusha kwa muziki mchangayiko wa DJ BonyLuv!