Katika jitihada za kuhakikisha TMA inashiriki kikamilifu katika kuongeza pato la Taifa, Mamlaka iliandaa mafunzo ya siku tano ambayo yalikuwa yana lengo la kutoa uelewa wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma katika kuboresha utendaji wa kazi hasa katika usimamizi na utekelezaji wa shughuli za ununuzi na usimamizi wa mikataba.

Akizungumza wakati akifunga rasmi mafunzo hayo, Mkurugenzi mkuu wa TMA, Dkt Agnes Kijazi alisema wakuu wa idara na vitengo wafanye maboresho kwenye maeneo yaliyokuwa na changamoto na kitengo cha ununuzi waboreshe utendaji wa kazi sambamba na kusimamia vizuri taratibu zote zinazohusu ununuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kama ilivyoelekezwa na washauri waelekezi kutoka PSPTB ili kuisaidia Mamlaka yetu kutekeleza sera na mikakati ya Serikali ya kupunguza gharama za ununuzi kwa lengo la kuboresha pato la Taifa.

Aidha Dkt. Kijazi aliishukuru Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kukubali kutoa wataalam katika upande wa sheria ya ununuzi na kuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo kila inapobidi.

Kwa upande wa Bodi ya utaalam wa ununuzi na ugavi Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Bwana Paul Bilabaye kwa niaba ya Mtendaji Mkuu alitoa pongezi kwa TMA kwa uamuzi wa kutoa mafunzo haya kwa Viongozi wanaohusika na utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi na Ugavi.

Mafunzo haya yamejenga uwezo kwa Idara tumizi, Kamati za tathmini, Kitengo cha Ununuzi na Ugavi pamoja na Bodi ya Zabuni katika kutekeleza majukumu yake.

Mafunzo hayo ya siku tano yamefanyika katika ukumbi wa mikutano, Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu, Wakuu wa idara na wakuu wa vitengo vyote pamoja na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Mamlaka ya Hali ya Hewa.


Imetolewa na

Ofisi ya Uhusiano

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...