Jovina Bujulu- MAELEZO

Kuwepo na mfumo wa stakabadhi ghalani kumekuwa ni mkombozi pekee kwa wakulima wadogo na wa kati kwa kuwawezesha kupata bei nzuri ya mazao yao, ukilinganisha na bei zilizokuwa zinatolewa na wafanyabiashara wanaponunua mazao yakiwa shambani kwa kutumia vipimo ambavyo sio sahihi.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya usimamizi wa Stakabadhi za Ghala imesema kuwa kabla ya mfumo huo kuanza wakulima walikuwa wakipunjwa bei ya mazao na wafanyabiashara na kutolea mfano zao la korosho ambapo katika msimu wa 2015/2016, kilo moja ya korosho ilinunuliwa kwa shilingi 2900 na msimu wa 2016/2017 bei ilipanda na kufikia shilingi 4,000 kwa kilo ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 15.9

Mfumo huo umewanufaisha wakulima kwa kutumia ghala ambazo ziliachwa kwa muda mrefu bila matumizi ambazo zimekuwa na tija kwa wakulima.

Kupitia ghala hizo zenye ujazo wa kuanzia tani 200 hadi 5000 na kuendelea wameweza kuhifadhi mazao yao vizuri na kwa ubora unaotakiwa kwa matumizi ya sasa nay a baadaye.

Aidha, mfumo huo umeongeza ajira kwa wakina mama na vijana hasa katika maeneo ya kuchambua, kupokea na kupanga mazao ghalani. Vijana wengi wameajiriwa kwa kazi ya kushusha, kupanga na kupakia mazao na wameweza kujiajiri katika kilimo baada ya kuona mfumo huo unavyofanya kazi vizuri na kuwa na uhakika wa soko la mazao yao.

Wakulima pia wamepata mafanikio kwa kuwa na uhakika wa vipimo vya mazao yao yanayohifadhiwa ghalani kupimwa kwa kilogramu na si vinginevyo ambapo kabla ya mfumo huo wakulima walikuwa wakiibiwa mazao yao kutokana na matumizi ya vipimo ambavyo si sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...