Tarehe 11 Aprili, 2017, Mhe. Balozi Wilson Mutaganywa Kajumula Masilingi aliwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico, Ikulu Katika Jiji la Mexico. 
 
Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mexico na mke wa Mhe. Balozi, Marystella Masilingi. Wakati wa kuwasilisha hati hizo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kuongea na Mhe. Rais wa Mexico na kumpa salam kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico akimpokea Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mexico. Katikati anaeshuhudia ni Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico. 
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico na Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, nchini Mexico.
Kutoka kushoto, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico; Mke wa Balozi Bi. Marystella E. Masilingi na Mhe. Luis Videgaray, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi na Mke wake Bi. Marystella Masilingi (kulia) na Bi. Swahiba Mndeme, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...