THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mila potofu – Kikwazo Matibabu kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi

Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Pham Dinh Quan (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wenzake kutoa zawadi kwa mmoja wa mama wa watoto wenye vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu ya Halotel, Stella Pius (kulia) na wafanyakazi wenzake wakitoa zawadi kwa mmoja wa mama wa watoto wenye matatizo ya vichwa vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)
Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel wakiwa katika picha ya pamoja nje ya wodi ya watoto ya Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kabla ya kutoa zawadi ya Pasaka kwa watoto hao.    

Wito umetolewa kwa jamii ya watanzania kuacha mila potofu inayopelekea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wenye matatizo mbalimbali hasa tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi bali wawapeleke hospitali mapema ili wapate matibabu kwani wanaweza kupona endapo wakiwahishwa hospitali.

Wito huo umetolewa na Afisa Mawasiliano mwandamizi wa Hospitali ya Mifupa (MOI) Bi. Mary Ochieng, wakati akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Halotel walipotembelea wodi za watoto hao pamoja na kutoa misaada ya kijamii, akizungumza na wafanyakazi hao Ochieng, amesema kuwa licha ya Taasisi hiyo kufanya jitihada kubwa za kutoa elimu na kufanya upasuaji kwa watoto hao bure bado kuna baadhi ya wazazi wameendelea na tabia ya kuwaficha watoto wao.

“Tangu Taasisi yetu ichukue jukumu hili imefanya kazi kubwa sana, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeweza kutoa matibabu kwa watoto wengi, ila changamoto kubwa bado inabaki kwa baadhi ya wazazi ambao wanawaficha watoto wao pale inapotokea wakagundua watoto wao wana matatizo ya vichwa vikubwa au mgongo wazi” Alisema nakuongeza.