Mratibu wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Elinasi Monga akifundisha somo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo aliweza kukazia suala la waandishi wa habari kujua visababishi na viashiria ambavyo ni vyema kujua na kuweza kuvifanyia kazi kwa ufasaha zaidi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog. Katika mafunzo hayo Mratibu wa Mradi huo alisema kuwa wakulima wadogo wadogo ndiyo wanaathika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa wamekuwa hawana uelewa mzuri katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi. Aliongeza jambo lingine linalorudisha nyuma ni serikali za mitaa kukosa mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Mwisho alisisitiza uongozi mbovu katika sekta ya misitu huchangia uharibifu wa misitu kwa kiasi kikubwa.
`
  Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Elinasi Monga akisisitiza jambo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akifundisha somo juu ya kiwango vya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, Nyenzo shirikishi pamoja na umuhimu wa misitu ya jamii ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...