1
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Bi. Asina Omary akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Woman And Youth Political Participation Enhanced In 2019 Aand 2020 General Election In Tanzania uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ,Serikalini. Vyama vya siasa, Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Asasi za Kiraia.

Mradi huo utakaotekelezwa na Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA na TYC na WE Effect huku ukifadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya kwa kiasi cha sh ilingi Bilioni 1.4na utatekelezwa kwa miaka mitatu.

Lengo la Mradi huo ni Kuongeza Ushiriki wa wanawake na vijana kwenye uwakilishi wa kisiasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2019-2020 katika ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi za vijiji hadi taifa, Mradi huu pia unalenga kuangalia vizuizi vinavyokwamisha wanawake na vijana kushiriki kwenye mchakato wa kugombea uongozi wa kisiasa na kuangalia ni jinsi gani vizuizi hivyo vinaweza kutatuliwa.
2
Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Roeland Van De Geer akitoa ujumbe wake kwa wageni waalikwa katika uzinduzi wa mradi huo, Jumuiya ya Ulaya ndiyo iliyofadhili mradi huo .
3
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA B. Athanasia Soka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...