Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye kupanda jukwaani na kuanza kuimba na kucheza kwa pamoja huku miluzi,shangwe na vigele gele vikiwa vimetawala uwanjani hapo.
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wananchi (hawapopo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema leo jioni jimboni kwake,kwenye uwanja wa shule ya msingi Kiwakala,mkoani Lindi.Mh Nape aliwashukuru Wananchi wake kwa kumpigia kura za kutosha na hatimae akachaguliwa kuwa mwakilishi wao Bungeni,akawashukuru kwa mapokezi makubwa waliompa na kumuonesha ni kiasi gani bado wanampena na kumuhitaji kama kiongozi wao mpambanaji katika kuwaletea maendeleo.

''Kilichonitoa machozi ni heshima kubwa mlionipa akina Mama,Mlilala chini,makataka nipite juu yenu,si ambalo nililitegemea,Nawashukuru sana,Niwaahidi nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote,kuwatumikieni,usiku na mchana,nitaikumbuka heshima hii mlionipa na sitoisahau",alisema Mh Nape huku sauti yake ikiendana na hisia ya kutoa chozi mbele ya umati mkubwa uliokuwepo pale uwanjani. 

Mh,Nape alizungumza mambo mbalimbali yakiwemo ya kuiletea maendeo jimbo la Mtama,kuzitatua changamoto zilizopo kama vile  Maji,Barabara,Elimu na Afya,amesema katika maeneo hayo atayasimamia kwa spidi kubwa kwa sababu amepata muda wa kutosha wa kuanza kuwahudumia wananchi wa jimbo lake na kuhakikisha anatimiza yale yote aliyokwisha waahidi wakati wa kampeni.

Pia amewataka Wananchi hao kuungana na kuwa kitu kimoja na kuweka itikadi za kisiaza pembeni na kuhakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha jimbo la Mtama linapiga hatua kimaendeleo.
Baadhi ya Wananchi na Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mbunge wa jimbo lao,Mh Nape Nnauye mapema jioni ya leo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akipita juu ya migongo ya baadhi ya akina Mama walioamua kulala chini ili kiongozi huyo apite juu yao,ambapo imeelezwa kuwa imefanywa vile ikiwa ni sehemu ya heshima kubwa waliompa pamoja na upendo walionao kwa Mbunge wao kwa kusimamia ukweli.Kitendo hicho kilisababisha Mh.Nape ashindwe kujizuia na kuanza kutoa machozi.
Sehemu ya Umati wa watu wakishangilia kwa pamoja mara baada ya Mh Nape kupanda jukwaani na kuianza kuimba nyimbo kwa pamoja huku wakicheza sambamba na shangwe za hapa na pale uwanjani hapo
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Nape,alipowasili jimboni humo mapema leo kwa lengo la kuwashukuru kwa Kumchagua kuwa mwakilishi wao mzuri na pia kuzungumza mipango yao mbalimbali ya kuliletea maendeleo jimbo lake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...