Basi la Kampuni ya Safari Njema lenye namba za usajili T 706 AMQ lilikuwa likitokea jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Dodoma, limepiga mweleka (pinduka) mapeka asubuhi ya leo katika eneo la Ruvu karibu na machining, Mkoani Pwani. Chanzo cha ajali hiyo hakikufahamika kwa haraka na inadaiwa kwamba Dereva wa basi hilo alitoweka kusikojulikana, Hakuna vifo katika ajali hiyo ila majeruhi ambao walipatiwa huduma ya kwanza na askari wa Zimamoto waliofika eneo la tukio muda mfupi baaada ya kupata taarifa na baadae kupelekwa hospitali ya rufaa ya Tumbi kwa matibabu zaidi akiwapo kondakta alievunjika mguu.
Muonekano wa basi hilo baada ya kupiga mweleka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...