Na Richard Mwaikenda 
Moto Umeibuka katika duka kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda duka hilo lilianza kuungua majira ya 8:30. Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana. 
Magari ya zimamoto na uokoaji yalijazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.
Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana walikimbia nje ya duka kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.
Duka hilo kubwa la kisasa lenye yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na giza nene ndani ya jengo lililotawaliwa na wingu kubwa la moshi uliosababishwa na moto huo.
Waokoaji walijitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini changamoto ilikuwa kubwa kutokana na vikwazo vya giza na moshi mnene.
 Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
 Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo

 Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto uliokuwa ukiwaka ndani ya jengo hilo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...