THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MICHUZI TV: OFISI YA RAIS TAMISEMI NA WABUNGE WAONGOZA MAZOEZI DODOMA KUMUUNGA MKONO MAKAMU WA RAIS KATIKA KUFANYA MAZOEZI


Ofisi ya Rais TAMISEMI na baadhi ya wabunge wameongoza vikundi vya Jogging Mkoani Dodoma kufanya mazoezi kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Sluhu Hassan wa kufanya mazoezi.


Akizungumza baada ya mazoezi hayo Afisa Tawala kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bibi Rose Lugendo amewaomba wakazi wa Dodoma wajitokeze kwa wingi kufanya mazoezi kwa afya zao na kuimarisha mahusiano baina yao.

“Napenda kuwashauri wakazi wa Dodoma kujiunga na Jogging Clubs na kuwa na Utamaduni wa kufanya mazoezi kwa Afya zao” alisisitiza Bibi Rose.

Kwa upande wake Mbunge Wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde amewaasa vijana kujitokeza kufanya mazoezi kila siku na sio kusubiri kufanya mazoezi mara moja kwa mwezi kwasababu mazoezi ni sehemu ya maisha.

“Vijana tumieni fursa hii kufanya mazoezi na kujenga afya zenu mazoezi yawe sehemu ya maisha yenu” alisisitiza Mhe. Lusinde.

Naye Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago amevipongeza vikundi vya Jogging Dodoma kwa kuleta mwamko wa mazoezi katika mkoa wao na kujenga desturi ya watu kupenda mazoezi na michezo.

Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Daniel Shija amewahakikishia ulinzi wanamazoezi na michezo kwa ujumla katika sehemu mbalimblai ambazo watakuwa wanafanya michezo.


 

Mbunge wa Buyungu Mhe. Kasuku Bilago(kushoto) Mbunge wa Kiwani (Zanzibar) Mhe. Abdalla Haji Ali (kulia) wakifanya mazoezi ya viungo katika katika viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma ikiwa ni kuunga mkono wito wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan wa kufanya mazoezi.
 Mratibu wa Michezo Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Salum Mkuya akizungumza navikundi vua Jogging Club wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Viwanja vya Kilimani Club Mjini Dodoma.