Na Veronica Simba - Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na ujumbe kutoka kampuni ya JUMEME inayojishughulisha na uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya jua.

Ujumbe huo ulijumuisha baadhi ya wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa na Leo Schiefermueller.
Ujumbe huo ulifika ofisini kwa Waziri Muhongo mjini Dodoma, kumweleza mipango na mikakati yao ya kuendelea na uzalishaji wa umeme wa jua katika maeneo ya Tanzania yaliyo nje ya gridi ya Taifa ya umeme.
Kampuni hiyo, inaendesha mradi wa kuzalisha umeme wa jua katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na imelenga kuwafikia watu milioni moja ndani ya Tanzania kupitia mitambo 300 katika vijiji vilivyo nje ya gridi ya Taifa ifikapo mwaka 2022.
Profesa Muhongo, kwa upande wake, aliwahakikishia JUMEME kuwa Serikali itawapa ushirikiano unaotakiwa ili kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata umeme kwa kutumia njia mbalimbali muafaka kama ilivyodhamiriwa.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Kampuni ya JUMEME, waliomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kuzungumzia masuala ya uzalishaji umeme wa jua. Kutoka kulia ni Leo Schiefermueller, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa na Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
 Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME, Leo Schiefermueller (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto). Wengine pichani ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto), akitoa maelekezo kwa Ujumbe kutoka kampuni ya JUMEME ambao ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa (kushoto) na Leo Schiefermueller kutoka Ujerumani (kulia). Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga.

Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya JUMEME, Leo Schiefermueller (kushoto), akifafanua jambo kwa Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (kulia). Pamoja nao pichani, ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT), Padre Dk. Thadeus Mkamwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...