Na Veronica Simba - Dodoma

Wawekezaji mbalimbali wamemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ofisini kwake mjini Dodoma na kumweleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali katika sekta ya nishati nchini.

Akizungumza na Waziri Muhongo, mwakilishi wa Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta aliwasilisha nia ya Kampuni hiyo ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Thomas Buonga akiwa ameambatana na Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya Umma wa Benki hiyo, Noella Kimaro, walimweleza Waziri kuwa wanaangalia fursa ya kuwekeza katika miradi ya sekta ya nishati.

Naye, mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer, akiwa amefuatana na Ofisa kutoka ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi, alisema nia ya kampuni yake ni kuwekeza katika sekta ya nishati hususan uzalishaji wa umeme kwa kutumia upepo.

Waziri Muhongo aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia kupata ushirikiano kutoka serikalini endapo watakidhi vigezo stahiki vya uwekezaji vilivyowekwa.
Kutoka kulia ni Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya umma katika Benki ya Stanbic, Noella Kimaro, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Thomas Buonga na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), walipomtembelea ofisini kwake Dodoma hivi karibuni na kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer (kushoto) na Ofisa kutoka Ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi (kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akimsikiliza mwekezaji kutoka Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta (kulia). Katikati ni Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary.
 Kutoka kulia ni Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya umma katika Benki ya Stanbic, Noella Kimaro, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Thomas Buonga na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), walipomtembelea ofisini kwake Dodoma hivi karibuni na kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiagana na Ujumbe kutoka Benki ya Stanbic, waliofika ofisini kwake mjini Dodoma, kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. Kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...