Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi magomeni “QUARTERS”, mradi ambao kwa asilimia kubwa unawagusa watanzania wa hali ya chini.
Aidha Rais Magufuli ameendelea kusisitiza juu ya ahadi aliyoitoa kwa wakazi 644 waliokuwa wakiishi maeneo hayo kupewa nyumba ambapo wataishi bure kwa muda wa miaka mitano.
Pia, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Msanifu Majengo Elvis Mwakalinga amesema ujenzi wa mradi huo umezingatia miundombinu yote iliyohitajika ambapo itakuwa na sehemu za makazi, biashara, maegesho ya magari na bustani ya kupumzikia.
Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo ujenzi wake ulianza rasmi Octoba mwaka jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na muwakilishi wa wananchi wakifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...